Njombe, Julai 24, 2025 – Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Njombe, Bw. Antony Granton, leo ametembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa lengo la kusaini kitabu cha wageni na kufanya mazungumzo mafupi ya kikazi.
Katika ziara hiyo, Meneja huyo alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ambaye alikuwa ameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Pindi Hazara Chana.
Bw. Granton alitumia fursa hiyo kueleza kuwa Benki ya NMB kupitia tawi lake la Njombe inaendelea kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi, huku ikilenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha mijini na vijijini kwa lengo la kuwainua kiuchumi wananchi wa mkoa huo.
Kwa upande wake, Mhe. Mtaka alimpongeza Meneja huyo kwa kazi nzuri inayofanywa na benki hiyo na kusisitiza kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na taasisi za kifedha kama NMB katika kukuza maendeleo ya jamii. Aliongeza kuwa uwepo wa viongozi wa sekta binafsi kama benki ni muhimu katika kujenga uchumi wa mkoa.
Mhe. Balozi Pindi Chana naye alitumia nafasi hiyo kupongeza ushirikiano unaoendelea kati ya Serikali na sekta binafsi, hasa katika maeneo ya huduma za kijamii na kiuchumi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.