Njombe, Julai 2025 – Mkoa wa Njombe unaendelea na maandalizi ya kushiriki kikamilifu katika Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Nane Nane mwaka 2025, yakiongozwa na kaulimbiu isemayo: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.”
Kupitia kauli hiyo, Mkoa wa Njombe unaonesha dhamira ya dhati ya kuchochea maendeleo ya sekta za uzalishaji kwa kushirikiana na wananchi, taasisi mbalimbali na sekta binafsi, kwa lengo la kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza kipato cha wananchi na kuchangia katika kukuza uchumi wa viwanda.
Maandalizi ya mkoa yamejikita katika kuonesha mafanikio ya wakulima, wafugaji na wavuvi, ikiwemo matumizi ya teknolojia mpya, mbegu bora, ufugaji wa kisasa na uboreshaji wa miundombinu ya masoko ya bidhaa.
“Njombe tupo tayari kuwaonesha Watanzania wote fursa zinazopatikana mkoani kwetu. Pindi maonesho haya yatakapofunguliwa rasmi tarehe 01 Agosti 2025 katika Uwanja wa John Mwakangale, jijini Mbeya — usikose kutembelea mabanda yote 6 ya halmashauri za Mkoa wa Njombe. Utashuhudia kwa macho mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, ambazo ni msingi wa uchumi wa wananchi wetu. Kupitia Nane Nane tunapata fursa ya kuhamasisha vijana, wanawake na jamii kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika mapinduzi ya kilimo.”
Mkoa wa Njombe unawakaribisha wananchi wote kujifunza, kuunganishwa na fursa, pamoja na kushuhudia mafanikio ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kupitia ushiriki wake wa mwaka huu kwenye maonesho hayo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.