Mafunzo ya Wadodosaji (Enumerators) kwaajili ya Utafiti wa hali ya Lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 na wanawake walio katika umri wa kuzaa yameanza rasmi leo tarehe 05 Februari 2024 na yatamalizika terehe 09 Februari 2024 ambayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF Njombe. Utafiti huu utahusisha taarifa za lishe na visababishi vyake ikiwa ni pamoja na Usafi wa Maji ya Kunywa na Mazingira pamoja na malezi na makuzi ya watoto.
Mafunzo hayo yana lengo la kuwezesha Wataalamu kufanikisha ukusanyaji wa taarifa bora na sahihi za utafiti ili kutambua ukubwa wa matatizo ya Lishe katika ngazi ya Wilaya na Halmashauri pamoja na sababu zinazochangia uwepo wa viwango vya juu vya tatizo la Udumavu.
Aidha, mafunzo hayo yamewakutanisha Maafisa Lishe wote wa Mkoa wa Njombe na Watoa huduma kutoka katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za Afya na yamefungiliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari akiwakilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Juma Mfanga.
Ikumbukwe kwamba Uhamasishaji wa Lishe bora Mkoa wa Njombe ulioungwa mkono na wadau mbalimbali akiwemo UNICEF unaendelea.
#Lishe ya Mwanao Mafanikio yake, #Njombe Tunaweza.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.