Njombe.
Kufuatia Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka uliofanyika Mwishoni mwa mwezi Januari 2024 katika eneo la Soko Kuu Njombe lililopo Kata ya Njombe Mjini, Wafanyabiashara wa sokoni hapo wametuma salamu za Shukrani kwa Mkuu wa Mkoa huyo kwa kuhamasisha wazazi na walezi wenye Watoto wadogo kwenye maeneo ya biashara ya soko hilo kuwapeleka Watoto eneo maalumu lililotengwa kwa lengo la kuwatunza na kuwafundisha maelekezo yake yametekelezwa asilimia 99.
Salamu hizo wamezituma mara baada ya Afisa Habari Msaidizi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Chrispin Kalinga leo Tarehe 13 Februari 2024 kutembelea soko hilo na kutazama utekelezaji wa Maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe kama yametekelezwa.
Ikumbukwe kwamba, wakati wa mkutano wa mkuu wa mkoa wa Njombe wa Kusikiliza na kuzitatua Kero kwenye eneo hilo Mhe. Anthony Mtaka alitoa maelekezo ya kuzitatua changamoto zilizokuwepo ikiwa ni Pamoja na Kuhakikisha Watoto wote wanapelekwa kwenye eneo lililo tengwa (Day Care), Soko hilo lifungwe angalau saa nne usiku, Uboreshaji miundombinu ya sokoni ikiwa ni Pamoja na Vyoo na taa maelekezo hayo yote yametekelezwa
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.