Madaktari bingwa wa Dkt. Samia Suluhu Hassan wapatao 30 wakiongozwa na Dkt. Jackline Ndanshau wamewasili Mkoani Njombe kwaajili ya kuanza kutoa huduma za matibabu ya Kibingwa na Bobezi kwenye hospitali zote za Wilaya na Halmashauri za Miji mkoani Njombe kuanzia tarehe 06 Mei hadi tarehe 10 Mei 2024.
Madaktari hao wamekaribishwa Mkoani Njombe na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda.
Wakati akizungumza na Madaktari hao mbele ya Wanahabari Mhe. Juma Sweda amesema kuwa, "Katika Maeneo yetu takwimu zimeionesha kupungua kwa vifo vya mama na mtoto, sisi kama Mkoa tuliamua kuwa sasa vifo vya mama na mtoto basi, na kama ikitokea basi lazima tuulize maswali kwanini, madaktari hawa tunaamini watagawa ujuzi wao kwa madaktari ambao wapo katika maeneo yetu".
Aidha, Mhe. Sweda akaongeza kwa kusema kuwa, "Mheshimiwa Rais ametoa fedha nyingi za kujenga vitu vya afya vipo takriban sita vipya, hivyo tunaomba Wizara ya Afya izidi kuwekeza katika kuwaleta madaktari kwenye maeneo yetu, Uwepo wa Hizi huduma za Kibingwa utarahisisha kwa kiasi kikubwa kuwafikia wananchi kwa ukaribu zaidi, na hivyo kupunguza gharama za usafiri kwa wanufaika,tunaendelea kusisitiza kuwa Tanzania ya sasa inahitaji huduma za Afya kuliko wakati mwingine na mabadiliko ya Teknolojia na Tabianchi ni vitu vinavyosukuma huduma ya afya kupewa kipaumbele, tunahitaji nguvu yenu wataalamu katika kuwekeza ujuzi mlionao kutoa huduma kwa wananchi ili kasi ya Teknolojia itusaidia kupamhana na maginjwa yanayoibuka.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.