Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari, ametangaza kuwa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa ngazi ya mkoa yatafanyika wilayani Makete. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wanaharakati wa haki za wanawake, pamoja na wananchi kwa ujumla.
Bi. Omari ameeleza kuwa mwaka huu, maadhimisho yataongozwa na kaulimbiu isemayo, "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji". Kaulimbiu hii inalenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuimarisha usawa wa kijinsia na kuongeza fursa za maendeleo kwa wanawake na wasichana.
Aidha amesema kuwa, maandalizi ya maadhimisho hayo yanaendelea vizuri, huku wakazi wa Makete wakihamasishwa kushiriki kwa wingi tarehe 8 Machi, 2025. Sherehe hizo zitahusisha mijadala, maonesho ya kazi za wanawake, pamoja na utoaji wa tuzo kwa wanawake walioleta mabadiliko chanya katika jamii
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.