Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Mabunge Duniani ( IPU)Mh. Dkt.Tulia Akson amewatakaWakulima nchini kuendelea kuzalisha na kuyapa thamani mazao yao kwa kufanya hivyo kutapanua sosko la kimataifa kuwa na uhakika wa kilimo.
Ameyasema hayo alipokuwa Mkoani Njombe katika ufunguzi wa Mkutano wa 28 wa Maadhimisho ya miaka 30 ya Mtandao wa vikundi wa wakulima Tanzania MVIWATA uliokutanisha Wakulima wadogo kutoka Mikoa ya Tanzania na Nchi mbalimbaliamabapo amesema ni wakati Mwafaka sasa kwa wakulima kuongeza tija ya uzalishaji ili kulisha Taifa mara dufu Zaidi.
“Tunatamani migogoro kati ya wafugaji na wakulima iishe nchi hii, tunatamani migogoro ya ardhi iishe nchi hii, itatuchukuwa muda lakini hatua zimeshaanza kuchukuliwa kwa maana ya kwamba vijiji kupimwa moja, vijiji kupanga matumzi bora ya ardhi,” alisema Dkt. Tulia.
Alifafanua kuwa, “Ardhi hii ikitengwa kwa ajili ya kilimo basi ifanye kazi ya kilimo na asiwepo mkulima wa kupora au hata kama si mkulima ni mfugaji basi asiwepo mfugaji ambaye anaporwa ardhi yake kwa hiyo mipango hiyo ipo na katika utekelezaji wa bajeti mwaka huu wa fedha 2023/2024 fedha hizo zimetengwa, na tutaanza baadhi ya maeneo,” alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa huduma hiyo itakapoanza na Mviwata watakuwa sehemu ya wafaidika kwa sababu changamoto ya wakulima na wafugaji pamoja na watu kuporwa ardhi itapungua.
Pia Spika Dkt. Tulia, aliwataka wakulima kuendelea kuzalisha sambamba na kuyapandisha thamani mazao yao kwani kufanya hivyo kutapanua soko la kimataifa na kuwa na uhakika na kilimo chao.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mh.Anthony Mtaka alitoa rai kwa wakulima kwamba licha ya kuzalisha mazao kwa wingi wambuke kwaandalia watoto wao chakula ambacho kimeongezwa virutubisho.
“Wakinamama na kinababa tunapozalisha bidhaa zetu za kilimo tukumbuke kutenga mlo uliobora nyumbani, mlo uliobora hautoi nje ni mboga za majani unazolima mwenyewe, ni parachichi unayolima mwenyewe ndiyo tunda ni mahindi unayolima mwenyewe ndiyo wanga, kuku unayefuga mwenyewe ndiyo protini,” alisema Mtaka.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), Ndugu Stephen Ruvuga alisema kuwa baadhi ya changamoto zinazowakabili wakulima ni pamoja na uwepo wa changamoto ya uporaji ardhi vijijini ambayo inaathiri wakulima wadogo.
“Kuna migogoro mbalimbali ya ardhi mengine ya wazi mengine inayofukuta chini kwa chini katika maeneo mbalimbali ikiwemo migogoro kati ya wawekezaji na wakulima wadogo, wafugaji na wakulima, kati ya taasisi za serikali na wakulima na tunaamini kwamba ardhi ni uhai na si bidhaa hivyo kama taifa lina kila sababu ya uhakikisha ulinzi wa ardhi kwa wakulima wadogo,” alisema Ruvuga.
Mmoja wa wakulima aliyeshiriki mkutano huo, Sara Kinyunyu aliiomba serikali kuwapa haki ya kumiliki ardhi ya kutosha ambayo ndiyo inawawezesha kuwa wakulima na sio kuwapa kipaumbele wawekezaji pekee.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.