KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MZEE MKONGEA ALLY ATAKA WAJASIRIIAMALI WADOGO WAPEWE KIPAUMBELE MRADI MPYA WA SOKO KUU LA NJOMBE
MIRADI mitatu imewekewa mawe ya msingi na mmoja kuzinduliwa katika Halmashauri ya Mji wa Njombe na mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu yote ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu jipya la wafanyabiashara mkoani Njombe ambao unagharimu shilingi bilioni 9 na mwingine ni wa kituo cha Afya cha Ihalula uliogharimu shilingi Milioni 900.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye soko hilo jipya, Kiongozi wa mbio za mwenge, Mzee Mkongea Ali alimtaka Mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri kuwapa kipaombele wajasiliamali wadogo kupata milango ya biashara na siyo vinginevyo.
"Mheshimiwa Mkuu wa wilaya wa Njombe, wajasiliamali wadogo wapewe kwanza milango ya biashara stalajii kuona Wafanyabiashara wakubwa ndiyo wanakuja kupewa milango ya biashara, siko hili ni zuri na la kisasa kitasaidia kuinua Uchumi wa mkoa wa Njombe," alisema Ali.
Wakati huohuo Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ameipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (NJUWASA) kwa kwenda sambamba na kauli mbiu ya ujumbe wa mbio za Mwenge wa kuhimiza utunzaji wa vyanzo vya maji, ambapo mamlaka hiyo imeweza kudhibiti uharibifu wa mazingira ya chanzo cha maji cha Kibena Howard kinachosaidia usambazaji wa maji kwenye hospitali ya rufaa ya halmashauri ya mji ya Kibena.
Alimtaka Mkuu wa wilaya ya Njombe,Ruth Msafiri kumwondoa mwananchi mmoja ambaye amelima mazao karibu na chanzo cha maji cha Kibena kwa kuzingatia sheria inayokataza wananchi wasilime katika chanzo cha maji ndani ya mita 60.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Njuwasa, Mhandisi John Mtyauli alisema chanzo cha maji Kibena Howard kimekuwa kikisaidia usambazaji wa maji safi katika hospitali ya Kibena pamoja na chuo cha uuguzi Kibena mkoani Njombe.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.