Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari ameongoza Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) kuhusu dharura ya magonjwa ya Mlipuko na Kipaumbele ni Kampeni ya chanjo ya Surua Rubela kilichofanyika leo tarehe 12 Februari 2024 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Mji Njombe.
Kikao kimewakutanisha Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Kamati ya Usalama (M), Viongozi wa dini, pamoja Wasimamizi wa Shughuri za Afya Mkoani Njombe ambao hao watakwenda kufanikisha kampeni hiyo ambayo kitaifa itaanza rasmi Februari 15, 2024 hadi tarehe 18 Februari,2024 kwa watoto wenye Umri wa miezi 9 hadi Chini ya Miaka Mitano
Lengo la kampeni hiyo ya chanjo ni kuwakinga watoto 94, 343 dhidi ya ugonjwa wa Surua/Rubella katika Halmashauri zote za mkoa wa Njombe.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.