Njombe – Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari, amewataka wanawake wa mkoa huo kuongeza juhudi katika kuongeza idadi ya watoto wanaozaliwa ili kusaidia kupunguza pengo la idadi ya watu, akisisitiza kuwa ongezeko la wakazi ni moja ya njia muhimu za kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akizungumza katika Sherehe ya Usiku wa Mwanamke iliyofanyika jana, Machi 9, 2025, katika ukumbi wa Jonson Hall, Bi. Omari alisema kuwa Njombe ni miongoni mwa mikoa yenye idadi ndogo ya watu, jambo linalohitaji mwitikio wa jamii, hususan wanawake, ili kuhakikisha kizazi kijacho kinakuwa na nguvu kazi ya kutosha kwa maendeleo ya taifa.
"Ni muhimu kwa jamii yetu kufahamu kwamba ongezeko la watu lina mchango mkubwa katika maendeleo. Tunapaswa kuhakikisha kuwa kizazi kijacho kinakuwa na nguvu kazi ya kutosha ili kuchochea ustawi wa kiuchumi na kijamii," alisema Bi. Omari.
Katika hafla hiyo, wanawake walihimizwa pia kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kuchangia katika ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.