Njombe, Mei 26, 2025 – Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omary, amewapokea rasmi madaktari bingwa 37 watakaotoa huduma za afya katika halmashauri sita za mkoa.
Madaktari hao bingwa wa Mhe. Samia Suluhu Hassan watatoa huduma katika maeneo mbalimbali ya utaalamu ikiwemo: magonjwa ya wanawake na uzazi, ukunga, afya ya watoto na watoto wachanga, upasuaji, magonjwa ya mfumo wa mkojo, ganzi na usingizi, magonjwa ya ndani, afya ya kinywa na meno, pamoja na uuguzi wa kiwango cha juu.
Kupokelewa kwa madaktari wa Mama Samia hawa ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe, hasa katika maeneo ya pembezoni ambayo kwa muda mrefu yamekumbwa na upungufu wa wataalamu wa afya.
Bi. Judica amesema kuwa ujio wa madaktari hao ni hatua muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi, na amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, na kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.