KATIBU Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari amewataka watumishi wa taasisi za serikali kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujitathimini katika utendaji wao.
Katibu tawala ametoa wito huo wakati akizungumza na watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo NSSF,PSSF,NIC,NHIF na LATRA katika kikao chenye dhumuni la kufahamiana na kujua namna ya kushirikiana kiutendaji katika ukumbi wa NSSF House mjini hapa.
Judica amewataka watumishi hao kutoa taarifa pindi kunapotokea changamoto ili ziweze kutatuliwa.
Pia amewapongeza watumishi kwa kuendelea kufanya kazi muda wa ziada na hivyo kutoa fursa kwa wananchi kuhudumia muda mwingi.
Awali akisoma taarifa mbele ya katibu tawala,meneja wa NSSF Ndugu Juma Mwita amesema kwa kipindi cha mwaka 2022-2023 wamefanikiwa kuandikisha waajiri 42 sawa na wastani wa asilimia 50% ya huku malengo yakiwani kuandikisha waajiri 84 kwa mwaka.
Amesema katika sekta rasmi wamefanikiwa kusajiri wanachama 2,770 sawa na wastani wa asilimia 95.7% ya lengo la kuandikishwa wanachama 2,892 kwa mwaka,wakati kwa kipindi cha July,2022-2023 jumla yawanachama 1,314 waliandikishwa ambapo ni sawa na wastani wa asilimia 96.05% yalengo la kuandikisha wanachama 1,368.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.