LICHA YA KUWEPO KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA SERIKALI WA MIAKA MITANO WA KUZIWEZESHA KIPATO KAYA MASKINI NCHINI,LAKINI KWA UPANDE WA MKOA WA NJOMBE ZAIDI YA VIJIJI NA MITAA MIA MOJA NA HAMSINI NA TANO VIMEKOSA FURSA HIYO LICHA KUWA NA SIFA ZA KUTAKIWA KUNUFAIKA NA MPANGO HUO.
HAYO YAMEBAINISHWA NA AFISA MIPANGO WA MKOA WA NJOMBE,JACHINDA CHANG’A WAKATI AKITOA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO HUO KWA KIPINDI CHA MIAKA MINNE ILIYOPITA MBELE YA KATIBU MKUU IKULU,AMBAE PIA NI MWENYEKITI WA KAMATI YA TASAF TAIFA DOKTA MOSES KUSILUKA,AMBAPO HADI SASA WANUFAIKA WA MPANGO HUO WAMEPATIWA ZAIDI YA BILIONI 14.5.
NAE MKUU WA MKOA WA NJOMBE KOMREDI CHRISTOPHER OLE SENDEKA AMEWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI MKOANI HUMO KUYASEMEA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KUTOKANA UTEKELEZAJI WA MPANGO HUO KWA WANANCHI,MPANGO AMBAO LICHA YA KUWAWEZESHA WANANCHI KWA KIPATO,LAKINI UMEJENGA MIRADI YA MAENDELEO ZAIDI YA THEMANINI KATIKA SEKTA YA ELIMU,AFYA NA BARABARA.
DOKTA MOSES KUSILUKA NI KATIBU MKUU IKULU,AMBAE PIA NI MWENYEKITI WA KAMATI YA TASAF TAIFA AMETOA NENO LA MATUMAINI KWA WANANCHI WA VIJIJI NA MITAA MIA MOJA NA HAMSINI NA TANO MKOANI NJOMBE AMBAVYO VIMEKOSA FURSA YA KUNUFAIKA NA MPANGO WA TASAF,AMBAPO VITAINGIZWA KATIKA AWAMU IJAYO YA MPANGO WA TASAF,,AMBAO UTATEKELEZWA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO.
NAO BAADHI YA WANANCHI WALIONUFAIKA NA MPANGO WA TASAF MKOANI HAPA AKIWEMO ARTHU MALEKELA WAMEUELEZEA MPANGO HUO KUWALETEA TIJA AMBAPO WAMEBORESHA MAKAZI YAO NA KUANZISHA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIUCHUMI.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.