Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Njombe ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Anthony Mtaka, Mei 15, 2025, imefika jijini Mbeya kwa ajili ya kutoa pole kwa Kamishna Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Mkoa wa Njombe, Bi. Felista Orden Sanga, kufuatia kifo cha mumewe, Orden Wilson Sanga. Marehemu alifariki dunia hivi karibuni na kuzikwa tarehe 09 Mei, 2025 katika makaburi ya Jijini Mbeya.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati hiyo, Mhe. Mtaka alieleza kuwa msiba huo si wa familia pekee bali umeigusa jamii nzima ya Mkoa wa Njombe, kutokana na mchango mkubwa wa Kamishna Sanga katika kulitumikia taifa kupitia Jeshi la Uhamiaji. “Tumetoka Njombe kwa heshima na mapenzi kuja kukupa pole wewe Felista. Tuko pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu, tukimuomba Mungu akupe faraja na nguvu ya kusimama tena,” alisema Mhe. Mtaka.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.