Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakiswa leo Machi 16, 2024 amewapokea Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Hiyo Mhe. Jackson Kiswaga wamekagua miradi ya maji inayotekelezwa Mkoani Njombe.
Pamoja na miradi mingine moja ya Mradi wa Maji uliotembelewa ni pamoja na Mradi unaotekelezwa Wilayani Ludewa ambao umejengwa katika kata ya Madope kijiji cha Luvuyo, mara baada ya kukamilika mradi huo utawahudumia wananchi wa Kijiji cha Luvuyo Wilayani Ludewa na Wananchi wa Wilaya ya Njombe ambapo Mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwishoni mwa mwaka huu kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.5
Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Maji Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Wakuu wa Wilaya, Kamati ya Usalama, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wameshiriki ziara hiyo.
Mhe. Kissa Ngwakisa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo mkubwa wa maji ambao utawanufaisha wananchi wa upande wa Wilaya ya Ludewa na Wananchi wa Wilaya ya Njombe hivyo kupunguza adha ya maji iliyokuwepo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.