Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna msaidizi wa Polisi Mahamoud Hassan banga tarehe 19 April 2024 amefanya sherehe ya kumuaga aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Makuri Imori.
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka ambaye amepongeza kazi nzuri ya Jeshi la Polisi wanazofanya huku akiwataka viongozi wakubwa kuhakikisha inapotokea nafasi ya kupandishwa vyeo Kwa askari wa wadogo basi waangaliwe ili kuweza kutengeneza viongozi wa baadae wa Jeshi Hilo, Mhe. Anthony Mtaka amewataka askari kufanya kazi kwa umakini na uadilifu mkubwa kutochezea kazi.
Kamanda Makuri Imori aliyeondoka ameshukuru kwa ushirikiano nzuri ambao mkoa wa Njombe wameuonesha tangu achaguliwe kwa kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe akasisitiza kuwa ushirikiano huo uendelee Kwa kamanda mpya na kuendelea kupendana na kuheshimina na kuzingatia kauli mbiu yetu ya Jeshi ya Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu.
Naye Kamanda aliyekaribishwa Mahamoud Banga. amesema Jeshi la Polisi litaendelea kushirikina kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha mkoa unakuwa salama na kupunguza matukio ya kiuhalifu ili mkoa wetu uendelee kuwa salama.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.