Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Judica Omari ameiasa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kufanya kazi kwa ukaribu na kushauriana vyema na mkaguzi wa ndani wa hesabu za serikali ili kuhakikisha kuwa hoja zote zinazotolewa na mkaguzi huyo zinafungwa kabla hata ya kuja mkaguzi wa nje.
Akizungumza hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka katika kikao cha baraza la Madiwani wilayani Ludewa kilicholenga kujadili majibu ya hoja na mpango kazi wa utekelezaji wa hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo katika halmashauri hiyo ilikuwa na hoja 19 huku hoja 7 kati ya hizo zikiwa zimefungwa kwa kipindi cha mwezi
Mei mwaka huu na kupelekea kusalia hoja 12.
Ameongeza kuwa kufanya kazi kwa ushiririkiano na mkaguzi wa ndani pia husaidia kuweka sawa taratibu mabalimbali ambazo zimekuwa zikikiukwa na kumrahisishia kazi CAG pindi anapokuja kufanya ukaguzi wake huku akiwasisitiza kufanya vikao vya kisheria na kujadili hoja zote ambazo zimekuwa zikiibuliwa.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sunday Deogratias amesema amepokea ushauri na maagizo hayo yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuleta matokeo mazuri kwa miaka ijayo.
" Yote yaliyozungumzwa nimeyapokea na
tunaahidi kwenda kuyafanyia kazi ili kuweza kupunguza idadi ya hoja kwa miaka ijayo ama ikiwezekana kutokuwepo hoja kabisa". Amesema Deogratius.
Amesema katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2021/2022 halmashauri hiyo ilikuwa na hoja 19 ambapo hoja 10 zimefanyiwa kazi na kufungwa na kubakisha hoja 9 huku hoja za miaka ya nyuma zikiwa ni hoja 6 ambazo hoja 3 zilifungwa na kubakiwa na hoja 3.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Wise Mgina amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo halmashauri hiyo imekuwa ikipata hati safi hivyo watahakikisha wanaendelea kupata hati hiyo safi kwa miaka mingine ijayo.
Hata hivyo katika kupitia hoja hizo kwenye kikao hicho idara ya ardhi imeonekana kuwa na hoja nyingi na hasa katika suala la urasimishaji, ikifuatiwa na idara ya mweka hazina, mazingira, idara ya afya, ujenzi pamoja na idara ya manunuzi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.