Moja ya madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu kutoka NCHI ya China, Dkt. Zhang Junqiao, ambaye amekuwa akitoa huduma za kitabibu kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe, ameshiriki kuchangia damu mara baada ya kumaliza kipindi chake cha kutoa huduma. Dkt. Zhang alikuja nchini Tanzania kama sehemu ya programu ya matibabu iliyoandaliwa na serikali ya China kwa kushirikiana na Tanzania, ambapo zoezi hilo lilizinduliwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Balozi Chen Mingjian.
Katika tukio hilo lililofanyika katika STENDI YA ZAMANI Njombe Mjini, Dkt. Zhang alichangia damu ambayo itasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wenye mahitaji ya damu. Akizungumza baada ya kuchangia damu, Dkt. Zhang alisema, "Nimeona umuhimu wa kuchangia damu kutokana na upendo wangu kwa wanadamu wote na kutambua kuwa damu inaweza kuokoa maisha. Nawasihi wananchi wa Njombe kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wengi zaidi."
Mpango huu wa madaktari kutoka China ni sehemu ya ushirikiano kati ya Tanzania na China, ambapo nchi hizo zimekuwa zikifanya kazi kwa pamoja katika kuboresha huduma za afya na miradi mingine ya maendeleo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.