Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omary ametoa wito kwa wataalamu wa Afya kahakikisha wanaimarisha huduma ya Chanjo ya HPV na Kutoa majibu ya Kitaaluma ili Kuepusha Taarifa za Upotoshaji.
Akizungumza na Wakazi wa Kata ya Uwemba iliyopo Tarafa ya Igominyi Katika Halmashauri ya Mji Njombe Wakati akizindua rasmi Zoezi la Utoaji wa Dozi Moja pekee ya chanjo ya HPV dhidi ya Saratani ya Mlango wa kizazi kwa Wasichana wenye Umri wa Miaka 9 hadi 14, Ameleeza Sababu za Mabadiliko ya ratiba ya Chanjo ya HPV kutoka Dozi Mbili hadi kuwa Dozi moja akisema kwamba tafiti za Kisayansi zimethibitisha kuwa Dozi moja ya Chanjo ya HPV inatosha Kutoa Kinga Kamili dhidi ya Maambukizi ya Virusi Vinavyo Sababisha Saratani ya Mlango wa Kizazi.
Bi. Judica Omary amesisitiza kuwa Mtoto asiyepata Chanjo ni hatari kwa maisha Yake na kwa Jamii inayomzunguka Kwani anaweza Kuambukizwa au Kuwaambukiza Wengine Ugonjwa kwa Kutokuwa na Kinga na Kusema, "Ni Jukumu la kila Mmoja wetu Kuhakikisha anakuwa Mlinzi wa Mwenzake."
Chanjo hiyo inatolewa kwa kiwango Cha zaidi ya Asilimia 80 kwa wasichana wenye miaka 9 hadi 14 waliopo Shule za Msingi na Wachache kutoka Shule za Sekondari.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.