Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari amefungua semina kwa watumishi wa umma Mkoani Njombe juu ya uwekezaji kwenye dhamana za serikali inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Bi Judica amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka huku akiwataka washiriki kusikiliza kwa makini mafunzo hayo muhimu ambayo yatakuwa msaada kwa watumishi na serikali kwa kuwa uwekezaji kwenye dhamana za serikali ni salama na wenye faida kubwa kwa mwekezaji na kwa serikali kwa kuiwezesha kupata mapato.
Benki kuu ya Tanzania kwa niaba ya serikali huuza dhamana za serikali ikiwa ni njia mojawapo ya kukopa fedha kutoka soko la ndani kwa makundi mawili, dhamana za serikali za muda mfupi treasury bill na dhamana za serikali za muda mrefu treasury bonds ambazo huuzwa kwanjia ya kufanya mnada kulungana na mpango wa ukopaji wa serikali kutoka masoko ya mahitaji ndani ndani ya nchi,bila kuathiri mikopo kwa sekta binafsi
Benki kuu ya Tanzania ni benki yenye wajibu wa kutunza fedha zote za serikali,kukusanya mapato yote yatokanayo na dhamana za serikali na hati fungani pamoja na kuluipa wadai na wawekezaji wote wa dhamana na hati fungani pia inazitumia dhamana za serikali na hati fungani kuleta uwiano kwenye ukwasi na ujazi wa fedha nchini Tanzania kama sehemu ya utekelezaji wa sera ya fedha.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.