MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA PILI YA MWAKA 2023/2024 WAFANYIKA LEO LUDEWA.
Na. Chrispin Kalinga - Njombe
Tarehe 03 Januari 2024 Madiwani wa Kata zote 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa wamefanya Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Robo ya pili ya Mwaka 2023/2024 wa Kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Disembai 2024 kwa Tarehe 03 Januari, 2024 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ukiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Mhe. Wise Mgina.
Aidha Mkutano huo umehudhuliwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mwakilishi wa Ktibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Reagan Mrosso, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Wakuu wa Divisheni na Vitengo pamoja na Wnanchi wa Wilaya ya Ludewa.
katika Mkutano huo zimewasilishwa taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudhibiti Ukimwi, Taarifa ya Kamati ya huduma za Elimu, Afya na Maji, Taarifa ya Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Taarifa ya Kamati ya huduma za Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Taarifa ya mradi wa kuboresha usalama wa Milki ya Ardhi.
Aidha, wakati akitoa salamu za serikali Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva, amewaomba watum,ishi wote wa wailaya ya Ludewa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwasihi kuwa na ushirikiano katika uwajibikaji wao.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.