Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan, amewasili mkoani Njombe kwa ziara rasmi, ambapo alipokelewa katika eneo la Makambako na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka. Mapokezi hayo yamefanyika asubuhi ya leo, huku viongozi mbalimbali wa serikali na sekta binafsi wakishiriki katika kumpokea mgeni huyo muhimu.
Baada ya mapokezi, Mhe. Balozi Avetisyan alielekea kwenye kiwanda cha AVO Afrika, ambacho kinasindika na kukamua mafuta ya parachichi. Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Urusi, hususan katika sekta ya kilimo na viwanda. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Balozi amesema kuwa Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa mikubwa inayozalisha parachichi kwa wingi nchini Tanzania, na akasisitiza kuwa parachichi za Tanzania hazitakumbwa na pingamizi lolote kuingia nchini Urusi.
"Njombe is one of the largest avocado-producing regions in Tanzania, and I can confidently say that Tanzanian avocados will face no obstacles in entering the Russian market. As the Russian Ambassador, I am now ready to bring Russian investors to Njombe to explore and invest, particularly in the areas of industrial development and modern agriculture," alisema Mhe. Balozi Avetisyan.
"Njombe ni moja ya mikoa mikubwa inayozalisha parachichi nchini Tanzania, na nina uhakika kwamba parachichi za Tanzania hazitakumbwa na vikwazo vyovyote kuingia katika soko la Urusi. Kama Balozi wa Urusi, sasa niko tayari kuwaleta wawekezaji wa Kirusi kuja Njombe kutazama fursa zilizopo na kuwekeza, hususan katika eneo la ujenzi wa viwanda na kilimo cha kisasa," alisema Mhe. Balozi Avetisyan.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.