SEKTA YA KILIMO
Mafanikio makubwa yameonekana katika Sekta ya Kilimo na hivyo kuboresha uchumi na maisha ya Wakulima. Maeneo yaliyoonesha ufanisi ni pamoja na:-
Wananchi wameendelea kupokea pembejeo za kilimo kwa njia ya ruzuku ambapo utaratibu huu umefanikisha upatikanaji wa pembejeo kwa urahisi na kuongeza tija. Mpango huu ulianzishwa mwaka 2006/2007. Katika kufanikisha mpango huu Serikali ilitoa ruzuku ya pembejeo za kilimo zenye thamani ya jumla ya shilingi 18,400,650,000/= kwa kipindi cha miaka miwili (2012/13 na 2013/14). Vocha hizi ziliwezesha eneo la hekta 95,129 kulimwa na kaya zipatazo 144,506 zilinufaika.
Uzalishaji wa mazao ya Chakula na Biashara umepanda na kufikia tani 1,713,189 kwa mwaka 2014 ikilinganishwa na tani 463,694 mwaka 2005. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 270. Ongezeko hili limetokana na tija ya uzalishaji ambapo kwa Mahindi uzalishaji uliongezeka kutoka wastani wa tani 2 kwa hekta hadi kufikia wastani wa tani 3 kwa hekta, Mpunga kutoka wastani wa tani 1.5 kwa hekta hadi kufikia wastani wa tani 2.5 kwa hekta, na viazi mviringo kutoka tani 11 kwa hekta hadi wastani wa tani 15.
Kwa miaka yote tisa Mkoa umeendelea kuwa na ziada ya mazao ya chakula na kuwa na usalama wa Chakula Mkoani. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2013/14 Mkoa una ziada ya tani 553,155 za nafaka na tani 248,519 za viazi Mviringo.
Eneo linalolimwa limeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Eneo la mazao ya Chakula limeongezeka kutoka Hekta 232,212 mwaka 2005 hadi Hekta 367,769 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia.58. Kwa upande wa mazao ya Biashara eneo limeongezeka kutoka Hekta 17,645 mwaka 2005 hadi Hekta 81,969 sawa na asilimia 365.
Utambuzi wa eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji limeongezeka kutoka
hekta 9,581 mwaka 2005 hadi kufikia hekta 18,101 mwaka 2014, sawa na
ongezeko la asilimia 89.
Eneo linalomwagiliwa limeongezeka kutoka hekta 2,281 mwaka 2005 hadi kufikia hekta 5,541 mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 143. Eneo la umwagiliaji lililoboreshwa limeongezeka kutoka hekta 856 mwaka 2005 hadi kufikia hekta 1,242 sawa na ongezeko la asilimia 45.
Huduma za ugani zimeboreshwa kwa kuongeza idadi ya Maafisa Ugani ambapo mwaka 2005 walikuwa Maafisa Ugani 172. Hadi kufikia mwaka 2014 Mkoa una juml
a ya Maafisa Ugani 363 sawa na ongezeko la asilimia 111. Aidha katika vijiji ambavyo havina Maafisa Ugani, Wagani kazi 240 wamepewa mafunzo na kufanya huduma za ugani vijijini ambapo Wagani kazi hao hawakuwepo mwaka 2005.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.