Katibu wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE Mkoa wa Njombe, Bi. Angel Chipindula, amewataka watumishi wapya kutumia haki yao ya kiutumishi kwa kujiunga na vyama vya wafanyakazi, akisisitiza kuwa vyama hivyo vina nafasi kubwa ya kutetea haki na kulinda maslahi ya watumishi.
Akizungumza katika mafunzo elekezi yanayoendelea mkoani Njombe, Bi. Chipindula alisema: “Nawasihi mtumie haki yenu ya kiutumishi kujiunga na vyama vya wafanyakazi. Vyama hivi vina uwezo wa kukaa na waajiri kwa ajili ya kutetea haki zenu au kwa namna moja ama nyingine kuwalinda dhidi ya changamoto za kikazi.”
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.