• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

IFAD YATAMBULISHA MRADI WA MAZIWA MKOANI NJOMBE.

Posted on: August 19th, 2025

Njombe, 14 Agosti 2025 – Shirika lisilo la kiserikali la IFAD likishirikiana na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi lilitembelea Mkoa wa Njombe na kufika katika ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, kwa lengo la kutambulisha Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi unaotekelezwa nchini Tanzania.


Wawakilishi wa IFAD walieleza kuwa mradi huo una dhumuni la kuboresha sekta ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kupitia matumizi ya mbegu bora na teknolojia za kisasa, kuongeza uzalishaji na kuinua kipato cha wafugaji wadogo. Aidha, walisisitiza kuwa mradi huo utajikita pia katika kushirikisha makundi maalum ya jamii, ikiwemo wanawake kwa asilimia 40, vijana 30 na watu wenye ulemavu kwa asilimia 3.


Akizungumza baada ya kupokea ujumbe huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari, aliwashukuru wadau hao kwa kuchagua Mkoa wa Njombe kuwa miongoni mwa mikoa ya mfano katika utekelezaji wa mradi. Alisisitiza kuwa utekelezaji wa mradi huo utakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo kupitia sekta ya maziwa, na kwamba serikali ya mkoa ipo tayari kushirikiana na wadau wote kuhakikisha unafanikiwa.


Mradi huu ulianza kutekelezwa mwezi Julai 2025 katika mikoa 8 ya Tanzania Bara na Visiwani mikoa 5, huku Mkoa wa Njombe ukiwa mmoja wa walengwa. Katika mkoa huu, utekelezaji unafanyika kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe  ukilenga kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa, kuimarisha mifumo ya ushirika na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • KATIBU WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI TUGHE MKOA WA NJOMBE AWASISITIZA WATUMISHI WAPYA KUJIUNGA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI.

    August 20, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE BI. JUDICA OMARI AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI WAPYA

    August 20, 2025
  • IFAD YATAMBULISHA MRADI WA MAZIWA MKOANI NJOMBE.

    August 19, 2025
  • NJOMBE: WAKUU WA IDARA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA MANUNUZI YA UMMA.

    August 18, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.