WAFANYAKAZI WA SERIKALI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII
"Chama cha Mapinduzi kimeonyesha njia na dira, ndugu zangu hatufuti upinzani, upinzani unajifuta wenyewe kutokana na kazi nzuri ya Magufuli anayoifanya na sisi tuliopo chini yake tunavyotekeleza," alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Mwamwala na kushangiliwa na wajumbe.
"Wajibu wetu ni vizuri tuasisi yale mambo anayofanya Rais wetu, mwenyekiti wetu wa chama, kufanya hivyo tutafauru, tutafika vizuri," alisema Mwamwala.
Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Njombe, aliwaeleza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Njombe kuwa hivi sasa wananchi wanaimani kubwa na CCM na ni vizuri wakaendelea kuwapa imani wananchi.
"Jana (juzi) tulikwenda na mkuu wa Mkoa kutembelea kundi dogo lakini ni kubwa la wafanyabiashara, kuzungumza nao ambao wameshika uchumi, hawa tuliona ni kundi ambalo limeachwa, halizungumzwi, halitembelewi, wajibu wetu ni kutembelea wananchi, taasisi na makundi mbalimbali," alisema Mwamwala.
"Tumekuta wana kero nyingi, ambazo tunatakiwa sisi tuzipe majibu, watu wale wamefurahi, wamefarijika wameona kuku mzazi mtetea amekwenda kuzalia mayai yake vizuri," alisema.
Awali Katibu wa CCM mkoa wa Njombe, Hosea Mpagike alisema kikao hicho kiliwakutanisha wajumbe wa siasa ya mkoa kujadili taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 pamoja na ya kuimarisha uchumi.
Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Njombe alifuatana na Wakurugenzi wa Halmashuari zote nne za mkoa wa Njombe pamoja na wataalam kutoka serikalini.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.