SERIKALI inatarajia kuanza ujenzi wa chuo kikuu cha masuala ya ndege
(Aviation) ili kuanza kuzalisha wataalam kutoka hapa nchini.
Tayari kiasi cha Dolla milioni 62 zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa chuo hicho.
Hayo yalibainishwa jana na waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
mhandisi Isack Kamwelwe ambaye yupo mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi
ya siku tatu akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mhandisi Kamwelwe alisema Tanzania tayari imeshanunua ndege saba na
nne tayari zimeshawasili hapa nchini lakini bado wataalam wa masuala
ya ndege wanalazimika kwenda kusoma nje ya nchi.
“Ili kukabiliana na changamoto hii ya wataalam wetu kwenda kusoma nje
na kwa kuwa tayari tunazo ndege zetu basi serikali imeona ni vyema
tukawa na chuo chetu kitakacho saidia kuzalisha wataalam wetu kutoka
hapa nchini,”alisema.
Kuhusu uwanja wa ndege wa Njombe mhandisi Kamwelwe alisema kati ya
viwanja 11 vinavyotarajiwa kukarabatiwa nchi nzima uwanja huo ni mmoja
wapo hivyo aliwataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki
ambapo serikali inajipanga ili kuanza kwa ukarabati huo.
Aidha mhandisi Kamwelwe alibainisha kuwa serikali imetenga kiasi cha
shilingi milioni mia 3 kwaajili ya ukarabati wa kipande kilichokuwa
kimechimbika katika kiwanja cha ndege cha Iringa ili kurahisisha
usafiri wa anga.
Alisema kiwanja cha ndege cha Iringa mwezi Septemba kitaanza kupokea
ndege za serikali aina ya bombadia ambayo itaanza kutua katika kiwanja
hicho kutoka jijini Dar es salaam.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.