SERIKALI INAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA –OLE SENDEKA
Wakazi wa Kijiji cha Lulanzi wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe wameshukuru kukamilika kwa ujenzi wa zahanati kijijini ambapo itawasaidia kupata huduma za afya karibu na makazi yao.
Wakizungumza na wakazi hao wamesema wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita 24 kufika hospitali ya mkoa hali iliyopelekea wazazi kujifungulia njiani.
Akizungumzia Adha hiyo mkazi wa kijiji cha lulanzi Upendo Wikunge,alisema kabla ya kukamilika kwa kituo hicho walikua wakipata huduma ya afya katika hospitali ya wilaya ya kibena.‘’awali hasa sisi wakinamama tulikua tunapata adha kubwa kwani kama mjamzito ikifika kipindi cha kujifungua ilikua inamlazimu kweda kibena ambako ni mbali takribani kilometa 24 ambapo umbali huu ulisabbaisha wazazi wengine kupoteza maisha’’alisema Upendo.
Zahanati ya lulanzi iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Kampuni ya Asas inayochakata Maziwa mkoani Iringa imezunduliwa na Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka pamoja na kampuni hiyo kukabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kujifungulia.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka alisema serikali imeendelea kuboresha huduma za afya mkoani humo kwa kutoa fedha ikiwemo Shilingi Milioni mia Nne katika kijiji cha Palangawanu wilayani Wanging’ombe.‘’Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya na ndio maana Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma TAMISEMI wameleta fedha katika kuboresha kituo cha afya cha parangawanu’’alisema Ole Sendeka.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha ASAS Fuhad Abri alisema uchangiaji wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Lulanzi ni hatua ya kuunga mkono serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.
‘’Tumengeza nguvu katika ujenzi wa zahanati hii ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto’’alisema Abri.Ujenzi wa zahanati hiyo umegharimu zaidi ya shilingi Milioni MIA MOJA kwa kushirikiana na vikundi vya wafugaji wa ngo’ombe wa maziwa vinavyofahamika Mshikamano.
Naye Mkuu wa wilaya ya wanging’ombe Ally Kassinge alisema sasa ni wakati wa ushirikiano kati ya serikali na wadau wengine katika kusaidia kuboresha huduma za afya wilayani humo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.