Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ameaza Ziara ya Kikazi Kuziangazia Fursa za Uzalishaji wa Mbegu Bora za mazao mbalimbali likiwemo zao la Parachichi.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameanza ziara ya kikazi yenye lengo la kuangazia fursa za uzalishaji wa mbegu bora mkoani Njombe. Katika ziara ya leo Januari 08, 2025, Mhe. Mtaka ametembelea vitalu vinavyozalisha mbegu bora za parachichi, mkoa unaojulikana kwa hali yake nzuri ya hewa inayofaa kwa kilimo cha matunda.
Akiwa kwenye vitalu vya Steven Mlimbila na Eligius Wella, wazalishaji wakubwa wa mbegu bora za parachichi, Mhe. Mtaka alielezea kuridhishwa kwake na juhudi za wakulima hao katika kuzalisha mbegu zenye viwango vya kimataifa. Alisisitiza umuhimu wa kilimo cha parachichi katika kukuza uchumi wa wakulima na mkoa kwa ujumla.
"Natoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja Njombe kuwekeza katika kilimo cha parachichi. Mbegu bora zinazalishwa hapa Njombe, na tunahakikisha mazingira bora kwa wawekezaji wote," alisema Mhe. Mtaka, akionyesha dhamira ya mkoa wa Njombe kuwa kitovu cha kilimo bora cha parachichi nchini.
Wakulima waliotembelewa walionyesha kufurahishwa na ziara ya Mhe. Mtaka, wakisema kuwa hatua hiyo itachochea ari ya uzalishaji na kuwavutia wawekezaji zaidi. "Ziara hii ni ishara ya kujali juhudi zetu, na tunaamini itasaidia kuongeza soko la parachichi za Njombe," alisema Eligius Wella.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.