Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Ndugu Elibariki Kingu, imefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe leo, tarehe 9 Januari 2025, na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ofisini kwake.
Ziara hiyo ya kamati ni ya siku mbili ambapo leo wametembelea Halmashauri ya Mji Njombe, na kesho, tarehe 10 Januari 2025, watakuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa afua mbalimbali za kupambana na maambukizi ya Ukimwi.
Akiwasilisha salamu za kamati, Ndugu Elibariki Kingu amempongeza Mhe. Mtaka kwa juhudi zake katika kuimarisha maendeleo ya Mkoa wa Njombe. Aidha, ameisifu kampeni ya mkoa dhidi ya udumavu inayobeba kauli mbiu isemayo "Kujaza Tumbo Si Lishe, Jali Unachokula" kwa kusema kuwa ni mfano mzuri wa jitihada za kuhakikisha afya bora kwa wakazi wa mkoa huo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.