• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

WAZIRI WA NISHATI DKT.MEDARD KALEMANI AIAGIZA TANESCO KUFANYA UTAFITI WA KINA KWA WABUNIFU WA UMEME WA MAJI MKOANI NJOMBE

Posted on: July 23rd, 2019

WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lifanye utafiti wa kina katika vijiji vya Msete na Lugenge ili kujua uwezo wa kasi ya maji yanayozalisha umeme wa maji uliobuniwa na wabunifu John Fuke maarufu Mzee Pwagu na Lainery Ngailo wenye nguvu ya kilovoti 28na kilovoti 15  ili kuwezesha vijiji vingine viweze kunufaika.

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani ambaye aliwatembelea wabunifu hao wa umeme wa maji, aliwasifu kutokana na namna walivyoweza kufanikisha kuzalisha umeme huo, lakini akatoa ushauri kwa mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuangalia uzalishaji wa umeme umeme huo unafanywa kwa kuzingatia  kisheria za nchi.

Awali mbunifu wa umeme wa maji mkoani hapa John Fute maarufu kwa jina la Pwagu alimweleza Waziri wa Nishati Dk. Kalemani kuwa jamii inayomzunguka imekuwa na shauku kubwa  ya kupata umeme anaouzalisha huku changamoto kubwa ikiwa ni ukosefu wa miundombinu bora na yenye uhakika katika kuwafikishia huduma hiyo.

Aidha katika hatua nyingine akiwa Wilayani Makete, Waziri wa Nishati Mh.Medard Kalemani aliwasha umeme katika shule ya msingi Kiduga iliyopo kata ya Ndulamo pamoja na kituo cha Afya na kuwataka wananchi kuendelea kuweka umeme wa gharama  nafuu wa REA Awamu ya Tatu kwa sababu serikali imedhamiria hivi sasa kila mwananchi apate umeme ili kuchochea kasi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mh.Christopher Ole Sendeka amesema wananchi wa mkoa wa Njombe wamenufaika na hatua ya muda mfupi ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano kuhusu upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme,ambayo imewawezesha wananchi kuanzisha na kuviendeleza viwanda vikubwa,vya kati na vidogo vidogo vikiwemo vya kusindika mazao mbalimbali.

Nao baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Regina Mgeni kutoka katika kata ya Ndulamo wilayani makete kwa upande wao hawakusita kutoa pongezi zao pongezi kubwa kwa serikali kuhusu hatua inazozichukua za kuwasogezea huduma ya umeme wa gharama nafuu(REA) katika vijiji wanavyotoka.



Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.