Watahiniwa 2,906 wanatarajiwa kufanya mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka huu Wilayani Makete Mkoani Njombe.
Mitihani inatarajiwa kuanza kesho tarehe 5 na kuhitimishwa tarehe 6 Octoba, 2022 katika vituo 104 kati ya hivyo vituo 102 ni vya Serikali na vituo 2 ni binafsi.
Akizungumza na Kitulo FM, Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda amewatakia heri wanafunzi wote wanaojiandaa na Mitihani hiyo.
Mhe. Sweda amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi hao kuwaandalia mazingira rafiki na kuacha tabia ya kuwarubuni ili wafanye vibaya mitihani yao kwani kufanya hivyo ni kumkosesha mwanafunzi haki yake ya msingi kutimiza ndoto zake.
Jumla ya Watahiniwa Milioni moja laki tatu themanini na nne elfu mia tatu arobani (1,384,340) wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi nchi nchini, kati ya watahiniwa hao 661,276 sawa na 47.77% ni wavulana na wasichana 723,064 sawa na 52.23%
Asilimia 95.74 ya watahiniwa hao ni sawa na 1,325,433 watafanya mtihani kwa Lugha ya Kiswahili na watahiniwa 58,907 sawa na 4.26% watafanya kwa Lugha ya Kiingereza.
Mkuu wa Wilaya amesema hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa katika vituo vyote vya kufanyia mitihani
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.