• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

WAKAZI WA KATA YA WANGING'OMBE MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUPATA TIBA SAHIHI KATIKA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VILIVYOPO,SAMBAMBA NA KUKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI WA KATA YA ILEMBULA UTASAIDIA KUONDOA KERO KWA WANANCHI

Posted on: September 19th, 2019


WANANCHI WA KATA YA WANGING'OMBE MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUTUMIA VITUO VYA AFYA,HOSPITALI KUPATA TIBA SAHIHI,SANJARI NA MRADI WA MAJI WA KATA YA ILEMBULA KUONDOA KERO YA MAJI PINDI UTAKAPOKAMILIKA

Wananchi wa kata ya wanging'ombe mkoani Njombe wamehimizwa kuacha hurka ya kukimbilia kutumia tiba za miti shamba na nyinginezo na badala yake watumie fursa ya uwepo wa hospitali na vituo vya Afya zaidi ya 300 vilivyojengwa nchini na serikali ya awamu ya tano kwani kwa kufanya hivyo  watakuwa wameunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli.

Rai hiyo imetolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Mzee Mkongea Ali wakati akiweka jiwe la msingi la majengo ya maabara, wodi ya wazazi, nyumba ya mtumishi pamoja na ofisi ya kuhifadhia taarifa muhimu za mahesabu zilizojengwa kutokana na fedha zilzilizotolewa na serikali zaidi ya shilingi Milioni 400.

"Na wasihi wananchi tutumie hospitali na vituo vya Afya vilivyojengwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli ili kumuunga mkono kwa kufuata huduma za matibabu za kitaalam kupitia wataalam waliosomea badala ya kukimbilia tiba mbadala isiyokuwa pengine bora," alisema Ali.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya,Francis Hoya alisema kuanza kutumika kwa majengo yaliyoanza kutoa huduma mbalimbali za matibabu kumepelekea kutoa huduma za upasuaji wa uzazi kwa wanawake 30.

"Kuwepo kwa utoaji wa huduma mbalimbali za Afya kwenye kituo hiki kimekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi na kuondoa tatizo la kufuata matibabu katika hospitali nyingine hapa wilayani," alisema Hoya.

Katika hatua nyingine, Mbio za Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Kata ya Wanging'ombe na Ilembula uliweka jiwe la msingi katika mabweni ya wanafunzi wasichana na wavulana wa shule ya Sekondari Wanging'ombe, huku kiongozi wa mbio za mwenge akiacha kuweka jiwe  la msingi katika mradi wa ujenzi wa tanki la maji la mradi uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 300 kutokana na mapungufu ya kiuhandisi .

Awali mkuu wa wilaya hiyo Ally Kasinge amesema kujengwa kwa mradi huo kutasaidia upatikanaji wa maji katika Kata ya Ilembula wilayani Wanging'ombe,na kuahidi kuyatafutia ufumbuzi mapungufu yote yaliyojitokeza ambapo unasimamiwa na mamlaka ya maji Wanging'ombe (Wangiwasa).

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.