Dodoma – Aprili 08, 2025
Maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Afya Kitaifa kwa mwaka 2025 yamefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, yakibeba kaulimbiu isemayo: "Tulipotoka, Tulipo na Tunapoelekea; Tunajenga Taifa Imara Lenye Afya." Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa afya kutoka taasisi mbalimbali.
Katika kuonesha mshikamano na ushiriki wa pamoja kwenye sekta ya afya, viongozi mbalimbali kutoka mkoa wa Njombe wameshawasili mapema kwa ajili ya kushiriki tukio hilo muhimu. Viongozi hao wanajumuisha watendaji wa kata, mitaa pamoja na maafisa waandamizi kutoka halmashauri mbalimbali za mkoa wa njombe. Ushiriki wao ni ishara ya kujitoa kwa dhati katika kuimarisha huduma za afya katika jamii wanazozihudumia.
Watendaji hao kutoka Njombe wanatarajiwa kushiriki kikamilifu kwenye mijadala na maonesho ya kisekta yanayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini. Aidha, wanatumia fursa hiyo kujifunza na kubadilishana uzoefu na wadau wengine wa afya kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwenye maeneo yao.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.