• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

TUMIENI BIDHAA ZILUIZOTENGENEZWA NCHINI ILI KUENDELEZA VIWANDA

Posted on: October 23rd, 2023

Naibu Waziri wa Viwanda na  Biashara Mhe. Exaud Kigahe  ametoa rai kwa Watanzania kupenda   na kunununua bidhaa  zinazotengenezwa na viwanda nchini ili kupanua wigo wa masoko ya bidhaa, kuongeza uzalishaji kukuza viwanda, kuongeza ajira na kipato cha mtu binafsi na pato la Taifa. Kigahe ameyasema hayo Oktoba 23, 2023 alipokuwa akifungua Maonesho ya nne (4) ya Shirika  Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba Mkoani Njombe kuanzia  21 - 31/ 10/2023 yakiongozwa na Kauli Mbiu isemayo  “Pamoja Tujenge Viwanda kwa Uchumi na Ajira Endelevu”.

"Niwahakikishie kuwa iwapo tutaunganisha kilimo na viwanda tutaweza kukuza soko la ndani lakini pia kupunguza uagizaji bidhaa ambazo tunaweza kuzizalisha sisi wenyewe kutokana na mazao ya kilimo na malighafi nyingine ambazo tunaweza kuzalisha ndani,lakini zaidi tutaweza kuingiza bidhaa zetu katika masoko ya nje na ya kimataifa"alisema Kigahe.

Alifafanua kuwa"Kwanza nyinyi ni mashahidi tunamasoko ya kikanda jumuia ya afrika mashariki bado hatujaitumia ipasavyo lakini jumuia ya maendeleo kusini afrika SADC bado hatujatumia soko lake vema, lakini zaidi sasa tunaeneo huru la biashara Afrika na huko kuna masoko mengi ya bidhaa nyingi na hasa zinazotokana na bidhaa zinazoongezwa thamani na mzao ya kilimo"alisema.

Kigahe alisema serikali imejipanga kuhakikisha inalisha dunia na afrika kwa bidhaa ambazo zimeongezwa thamani."Sio kuuza nje Parachichi kama ilivyo,kuuza Mahindi kama yalivyo,Alizeti na mengineyo,tuuze unga,tuuze bidhaa zilizoongezwa thamani,tuwalishe chakula ambacho kimeongezwa thamani kutoka Tanzania"alisema Kigahe.

Aidha amelitaka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO kushirikiana na Halmashauri ili kuhakikisha vijana wanapata teknolojia ili kuweza kifanya kilimo kibiashara. Katika hatua nyingine, ameishauri SIDO  kuendelea kuratibu Maonesho hayo Kitaifa kufanyika Mkoani Njombe kila mwaka kama ilivyo vya Sabasaba kitaifa kila mwaka ni Dar es Salaam , Dhahabu ni Geita kwa kuwa Maonesho hayo yanaonyesha taswira nzima ya bidhaa za kitanzania teknolojia, ubunifu,Mafanikio ma fursa kwa Mtanzania kutumia na kupanua wigo wa Uzalishaji.

Meneja mahusiano mwandamizi huduma za benki kwa serikali NMB Josephine kulwa,alisema maonesho hayo ni fursa kwa wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara mkoani Njombe ili kupata elimu ya mambo mbalimbali ikiwemo huduma zinazotolewa na benki ya NMB.

"Lengo la kudhamini kuhamasisha maonesho haya ni kutoa fursa kwa wajasiriamali,wakulima,wafanyabishara waweze kufahamu uwepo wa maonesho haya,benki ya NMB ambacho tumekuja nacho hapa kwanza tunatoa elimu ya ujasiriamali,tunatoa elimu ya kufedha na kukuwezesha kuona jinsi gani unaweza kukopesheka na mabenki mbali mbali hasa kwa upande wa benki ya NMB tunafanya mikopo mbalimbali kwa wajasiriamali ikiwemo mkopo wa mshiko fasta"alisema Josephine.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka,Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa alimshukuru Rais Samia kwa kutoa ruzuku kwenye mbolea ili kuongeza uzalishaji kwenye mazao ya chakula.

"Kwa sababu kwa kutoa kwake ruzuku imetusaidia kuongeza uzalishaji wa chakula na uzalishaji wa mazao ya kibiashara hivyo naamini maonesho haya yatatusaidia teknolojia ndogondogo ambazo zitatusaidia kuchagiza uzalishaji katika katika mkoa wa Njombe"alisema Kissa.

Mkurugenzi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO mhandisi Prof.Sylivester Mpanduji,alisema wamejipanga kutoa elimu kupitia simu za mkononi ili kuwafikia watanzania wengi zaidi ambao watahamasika kuanzisha viwanda.

Vilevile, ameielekelza Wakala wa Maendelo ya Viwanda Vidogo na vya Kati.(SMIDA) kushirikiana na SIDO katika kupata teknolojia na kuwawezesha vijana wa Zanzibar kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji ili nao waweze kuitumia fursa ya uwepo wa AFCFTA, EAC, SADC, AGOA na fursa nyingine za masoko ya pamoja.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.