• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATOA MCHANGO WA SHILINGI MILIONI 35 KUKAMILISHA KANISA LA AGRICAN MAKAMBAKO.

Posted on: December 29th, 2024

Makambako, Desemba 29, 2024: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa mchango wa shilingi milioni 35 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa la Agrican lililopo mjini Makambako. Mchango huo umewasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, akimwakilisha Rais Samia, katika hafla iliyofanyika leo kanisani hapo.

Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Rais, Mhe. Mtaka amesema kuwa Rais Samia amewapongeza viongozi wa dini kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kusaidia maendeleo ya kijamii, ikiwemo kusimamia maadili na kuwaongoza waumini kuwa raia wema. "Madhehebu ya dini na viongozi wa kidini mnafanya kazi kubwa sana ya kusaidia maendeleo ya nchi yetu. Endeleeni kuliombea mema taifa letu na kusimamia maadili kwa waumini wenu," amesema Mhe. Mtaka kwa niaba ya Rais.

Aidha, Mhe. Rais kupitia Mhe. Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe kuhusu umuhimu wa kuepuka tabia ya kujichukulia sheria mkononi, kitendo kinachopelekea mauaji na ukatili wa kijinsia. Pia, amesisitiza umuhimu wa kuhimiza lishe bora ili kutokomeza tatizo la udumavu linaloikumba mkoa huo.

Zaidi ya shilingi milioni 60 zimepatikana kupitia hafla hiyo, ambapo wachangiaji wengine wameungana na Mhe. Rais kuchangia tukio hilo. Mchango huo umeleta matumaini makubwa kwa waumini wa Kanisa la Agrican Makambako.

Akitoa shukrani, Askofu wa Kanisa hilo, Mhe. Matthew Mhagama, amesema, "Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla hii kupitia mwakilishi wake na kwa mchango wake wa shilingi milioni 35. Pia, tunawashukuru viongozi wote walioshiriki katika hafla hii na kuchangia, kufanikisha jumla ya zaidi ya shilingi milioni 60. Mchango huu utasaidia sana kukamilisha ujenzi wa kanisa letu."

Hafla hiyo imehitimishwa kwa dua ya shukrani, huku waumini wakionyesha furaha na shukrani kwa jitihada za pamoja katika kufanikisha maendeleo ya kiroho na kijamii.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.