Mwenge wa Uhuru Umewasili Mkoani Njombe Ukitokea Mkoani Ruvuma ambapo makabidhianao hayo yamefanyika katika Kijiji cha Ngelenge kata ya masasi Wilayani Ludewa baina ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Mh.Bi. Judica Omari na Steveni Mashauri ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma. Ambapo utakimbizwa katika Wilaya Nne zenye Halmashauri Sita za mkoa wa Njombe huku miradi yenye thamani zaidi ya shillingi billioni tisa nukta tatu ikitarajiwa kukaguliwa kuwekewa mawe ya msingi Pamoja na kuzinduliwa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omary akizungumza katika makabidhiano hayo Ameeleza kuwa Kauli mbinu ya Mwenge wa Uhuru 2023 imezingatia umuhimu wa mabadiliko ya Tabia nchi katika uhifadhi wa mazingira sambamba na utunzaji wa vyanzo vya maji.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Njombe umefanikiwa na kuendeleza mikakati ya utunzaji wa mazingira husasani upandaji wa miti ambapo mkoa huo umevuka lengo la kupanda miti Zaidi ya Milioni Hamsini kuanzia mwaka 2022 hadi kufikia mwaka huu ambapo tofauti ya lengo lililowekwa la kupanda miti milioni tisa kwa mwaka mmoja.
“Mkoa wetu unazaidi ya vyanzo elfu tatu vya maji ambavyo tunaendelea kuvitunza na kuvihifadhi kwa kuendelea kupanda miti ambayo ni rafiki na mazingira” Alisema Judica
Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimeanza kwa kukimbizwa katika Wilaya ya Ludewa ambapo umefanikiwa kuweka mawe katika vyumba viwili vya madarasa ya msingi katika shule ya Msingi Ngelenge,kuzindua vyumba vya kulala wageni,kuzindua klabu ya wapinga Rushwa,kukagua shambala korosho la wananchi,Kufungua Zahanati ya Kimelembe,kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri,miradi yote yenye thamani ya bilioni mbili milioni mia mbil arobaini na mbili. umekimbizwa katika Kilomita 173 ndani ya Vijiji nane
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa amekiri kupokea maelekezo kutoka kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote kama yalivyotolewa.
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya amemshukuru jitihada zinazoendelea kufanya na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea wananchi wa ludewa maendeleo mbalimbali ikiwemo huduma ya Afya katika Zahanati ya Kimelembe ambapo alipiga goti mbele ya wakimbiza mbio za mwenge kitaifa kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa Zahanati hiyo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.