Mh. Antony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe amefanya mkutano na Msemaji Mkuu wa Serikali pamoja na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita Mkoani Njombe amesema,Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh, Dkt. Samia Suluhu Hassan imewasikia wananchi wa Njombe na kuwafikia katika kutatuta kero zao kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Maji, Barabara, Kilimo, Elimu na Afya.
Kwa upande wa miundombinu ya barabara na maji, ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwakuwa Mkoa wa Njombe ni moja ya Mikoa inayonufaika na mradi mkubwa wa maji ambao utatatua changamoto ya maji kwa wananchi kwa asilimia 95, pamoja na miradi ya barabara ambapo ameishukuru serikali kwa kuboresha mtandao wa barabara na kufanya maeneno mengi ya Mkoa wa Njombe kufikika kwa kuwa na barabara zenye kiwango cha lami.
Aidha ameipongeza Serikali na maono ya Rais Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuona Umuhimu wa kulipa fidia ya bilioni 15 kwenye maeneneo ya makaa ya mawe na madini ya chuma Wilayani Ludewa sambamba na ujenzi wa barabara kubwa ya zege ambayo itafungua kwa kiasi kikubwa uchumi wa Wilaya ya Ludewa na Mkoa wa Njombe kwa Ujumla.
Pia ameipongeza Serikali kwa kutoa mbolea za ruzuku kwa wakulima jambo ambalo litasaidia kuendelea kuinua uchumi wa wananchi Njombe na kusaidia kuchangia kwenye pato la Mkoa na Taifa.
Mh. Mtaka ameeleza namna Serikali ilivyofanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu jambo ambalo ni ishara ya mageuzi makubwa kwenye Elimu Mkoani Njombe kwakuwa kila kata Mkoani Njombe ina shule, hivyo kuwezesha Watoto wote wanaofaulu kuweza kuendelea na masomo.
Pia kwenye sekta ya Afya Mh. Mtaka ameishukuru Serikali ya awamu sita kwa namna ambavyo imesogeza huduma karibu na wananchi na Vifaa, Mdawa, watumishi na vitendea kazi vingine vinavyowezesha huduma kupatikana wakati wowote.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.