Jumla ya miti milioni sita kati ya miti milioni thelathini na moja iliyopandwa katika msimu uliopita Mkoani Njombe imeripotiwa kufa kutokana na shughuli za kibinadamu zisizozingatia uhifadhi wa mazingira.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa upandaji miti kimkoa uliofanyika katika Soko la Kiumba, katika mji wa Makambako, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Mhe. Zakaria Mwansasu amewaagiza watendaji wa serikali katika ngazi zote kuhakikisha miti inayopandwa inalindwa na kutunzwa ipasavyo ili kufikia lengo la uhifadhi endelevu wa mazingira.
Mwansasu amesema Mkoa wa Njombe umeweka mkakati wa kila Halmashauri kupanda angalau miti milioni tano kwa mwaka, hatua inayolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kulinda vyanzo vya maji pamoja na kuimarisha uchumi wa wananchi.
Pia ameeleza kuwa upandaji miti ni muhimu kwa ustawi wa mazingira, afya ya binadamu na maendeleo ya vizazi vijavyo, huku akisisitiza wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo badala ya kuliona kama jukumu la serikali pekee.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.