Kikao cha tathimini ya utekelezaji wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira Mkoa wa Njombe kinaendelea muda huu katika Ukumbi wa Milimani Hotel uliopo njombe mjini, kikao hicho kimewakutanisha Maafisa Afya kutoka Halmashauri zote za mkoa wa Njombe.
Pamoja na mambo mengine zinawasilishwa taarifa mbalimbali za usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira, Taarifa ya Utekelezaji wa Udhibiti wa taka ngumu, Mfumo wa mnyororo wa utupaji wa kinyesi pamoja na Taarifa ya Mwelekeo wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira Mkoa wa Njombe.
Kikao hicho kinaongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.