• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

KATIBU TAWALA AZINDUA BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA.

Posted on: January 25th, 2025


Njombe, Tanzania – Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari, amemwakilisha Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka, katika uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, hafla iliyofanyika Januari 23, 2025.


Bodi hiyo, yenye jumla ya wajumbe tisa, imepewa jukumu la kuleta mapinduzi katika sekta ya afya mkoani humo kwa kipindi cha miaka mitatu. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Bi. Judica amesisitiza umuhimu wa Bodi kuhakikisha usimamizi bora wa huduma za afya, kuibua miradi ya maendeleo, na kushirikiana na uongozi wa hospitali katika utekelezaji wa mipango mbalimbali.


Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Danford Mpumilwa, ameahidi kuwa chombo hicho kitakuwa kichocheo cha maendeleo makubwa kwa kipindi chao cha utumishi. “Tuwajibike na kuifanya hospitali hii kuwa ya mfano hapa nchini kwa mawazo chanya yatakayosaidia katika ujenzi wa taasisi hii,” alisema.


Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Gilbert Kwesi, ambaye pia ni Katibu wa Bodi, amesema ushirikiano kati ya wajumbe na uongozi wa hospitali utakuwa nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya taasisi hiyo.


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Juma Mfanga, ametumia fursa hiyo kuitaka Bodi kuunga mkono juhudi za kupambana na udumavu mkoani humo. Wajumbe wa Bodi, walioteuliwa na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, wameshapatiwa mafunzo maalum kuhusu majukumu yao na ushirikiano unaotakiwa na timu za uendeshaji wa huduma za afya katika ngazi mbalimbali.


Mafunzo hayo yalihusisha muktadha wa kihistoria wa sekta ya afya kabla na baada ya uhuru, muundo wa uendeshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, na wajibu wa Bodi katika kusimamia maendeleo ya hospitali hiyo.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.