Wakulima wa zao la parachichi wameiomba Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha kupata teknolojia za kisasa zinazolingana na wakati. Wamesema hatua hiyo itawasaidia kukabiliana na changamoto za magonjwa na upungufu wa elimu sahihi kuhusu kilimo cha parachichi, zao ambalo limekuwa mkombozi wa kiuchumi kwao.
Katika mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Wadau wa Parachichi Tanzania (ASTA), wakulima walieleza matarajio yao ya kuona kilimo hicho kikibadilika na kuleta tija zaidi. Mwenyekiti mpya wa ASTA, Emmanuel Kisinda, alisisitiza kuwa jumuiya yake itasimamia kikamilifu ujenzi wa kiwanda kipya cha kuchakata mafuta ya parachichi, ambacho kinatarajiwa kukamilika kabla ya mwaka 2026. Aliongeza kuwa ASTA itaendelea kuhamasisha ongezeko la wanachama, ambapo kwa sasa jumuiya hiyo inajivunia zaidi ya wanachama 3,000 wakiwemo wakulima.
Kwa upande wa Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mhe. Zacharia Mwansasu, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe.Anthony Mtaka, amesema Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali kuhakikisha parachichi linapata thamani sokoni. Alisisitiza umuhimu wa wazalishaji wa miche ya parachichi kuzalisha miche bora yenye viwango ili kuongeza ubora wa uzalishaji na kuimarisha ushindani wa zao hilo kimataifa.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.