• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

Hotuba ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Ndg. Sunday Deogratias alipokutana na Viongozi wa Dini, Vyama vya Kisiasa, Wazee Maarufu, Watumishi na wananchi kutoa Maelekezo ya Uchaguzi

Posted on: September 27th, 2024

Mahali: Ukumbi Mdogo wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya LudewaTarehe: 26 Septemmba 2024

Ndugu Waandishi wa Habari,Waheshimiwa Viongozi wa Dini,Waheshimiwa Viongozi wa Siasa,Ndugu wananchi wa Wilaya ya Ludewa,Mabibi na Mabwana,

Asanteni sana kwa kujitokeza kwenye kikao hiki muhimu kinachohusiana na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Tunakutana hapa leo tukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa uchaguzi huu unakuwa wa amani, haki, na unaleta matokeo yanayoakisi matakwa ya wananchi wetu.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni fursa muhimu kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya maendeleo ya wilaya na taifa kwa ujumla. Serikali za Mitaa ndizo zinazosimamia huduma za msingi kama vile afya, elimu, maji, na miundombinu. Ni muhimu kwa viongozi watakaochaguliwa kuwa na dira na maono ya kuendeleza huduma hizi na kuboresha maisha ya wananchi wa Ludewa.

1. Umuhimu wa Ushiriki wa WananchiNingependa kutoa wito kwa wananchi wote wa Ludewa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huu utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Serikali yetu imeweka mazingira rafiki na kuhakikisha kuwa kila raia anapata haki yake ya kupiga kura kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na wenyeviti wa vitongoji za mwaka 2024. Ni haki ya msingi ya kila mwananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika kuamua nani atakayewaongoza kwenye ngazi za serikali za mitaa.

Kila mwananchi mwenye sifa za kupiga kura anatakiwa kutumia haki yake hiyo ya kupiga kura na vigezo vya wapiga kura waliojiandikisha.

2. Amani na Utulivu Kabla, Wakati, na Baada ya UchaguziViongozi wa dini, viongozi wa siasa, na vyombo vya habari, mna jukumu kubwa katika kuhakikisha kuwa tunadumisha amani kabla, wakati, na baada ya uchaguzi huu. Mna ushawishi mkubwa kwa wananchi na wafuasi wenu, hivyo ni muhimu kutoa ujumbe wa kujenga mshikamano, umoja, na kuepuka uchochezi wa aina yoyote.

Tunawataka wagombea wote na wafuasi wao kuhakikisha kuwa kampeni zitaendeshwa kwa sheria na kanuni zilizopo. Kila mtu ana jukumu la kuhakikisha kuwa sheria hizi zinaheshimiwa ili kuepuka vurugu na kuendeleza amani.

Nawaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani na ushirikiano miongoni mwa wananchi. Waandishi wa habari, ninyi ni sauti ya umma, naomba muendelee kuripoti kwa haki, ukweli, na bila upendeleo. Viongozi wa kisiasa, muwe mfano bora kwa kuepuka maneno ya uchochezi na badala yake muwaongoze wafuasi wenu kwa busara na hekima.

3. Maandalizi ya UchaguziNinafuraha kuwafahamisha kuwa maandalizi ya uchaguzi huu yanaendelea vizuri. Serikali imeweka mikakati thabiti kuhakikisha kuwa vifaa vya uchaguzi vinawafikia wapiga kura kwa wakati na mchakato mzima unafanyika kwa uwazi na ufanisi. Kila kitu kiko tayari kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa utaratibu na salama.

Sote kwa pamoja tunalo jukumu la kuhakikisha kuwa mchakato mzima wa uchaguzi unafanyika kwa uwazi na kwa mujibu wa sheria. Hivyo, wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu haki na usawa wa uchaguzi huu.

Ninawahakikishia kuwa sisi kama Halmashauri tutatekeleza wajibu wetu kwa mujibu wa sheria, kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki, na unaendeshwa kwa misingi ya uwazi na usawa. Hivyo basi, naomba tushirikiane kuhakikisha mchakato huu unafanikiwa.

4. Mwito wa UshirikianoNapenda kumalizia kwa kutoa mwito wa ushirikiano. Waandishi wa habari, viongozi wa dini, na viongozi wa siasa, tuendelee kushirikiana kwa karibu kuhakikisha uchaguzi huu unafanikiwa. Pamoja, tunaweza kudumisha amani, umoja, na mshikamano ili wilaya yetu ya Ludewa iendelee kuwa mfano wa kuigwa katika mchakato wa kidemokrasia nchini.

Ndugu zangu, uchaguzi ni sehemu ya maendeleo, na tusiruhusu tofauti zetu za kisiasa ziharibu amani na utulivu wetu. Amani ni nguzo ya maendeleo, na uchaguzi ni fursa ya kuboresha maisha yetu.

Asanteni kwa kunisikiliza, na nawatakia maandalizi mema ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Ahsanteni Sana.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.