Waratibu wa lishe kutoka idara mtambuka za Afya, Kilimo, Mifugo, na Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, wamefanya ziara ya mafunzo mkoani Njombe kwa lengo la kujifunza utekelezaji wa afua za lishe.
Ziara hiyo imehusisha kutembelea Halmashauri za Wilaya ya Njombe na Makete, ambapo waratibu hao walipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali za miradi ya lishe inayotekelezwa katika maeneo hayo. Kupitia ziara hiyo, washiriki wameongeza ujuzi na maarifa kuhusu mbinu bora za utekelezaji wa afua za lishe, kwa lengo la kuboresha huduma hizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Aidha, waratibu hao wameeleza kufurahishwa na mapokezi mazuri waliyopata kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe pamoja na Halmashauri za Makete na Njombe. Wameshukuru kwa ushirikiano mkubwa waliopata, ambao umewezesha ziara hiyo kufanyika kwa mafanikio makubwa.
Ziara hii ni sehemu ya jitihada za kuboresha afya ya jamii kupitia afua za lishe endelevu, kwa kuhamasisha ushirikiano kati ya halmashauri na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.