• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

HALMASHAURI SHIRIKIANENI NA WAKAGUZI WA NDANI

Posted on: June 17th, 2023

Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Judica Omari ameiasa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kufanya kazi kwa ukaribu na kushauriana vyema na mkaguzi wa ndani wa hesabu za serikali ili kuhakikisha kuwa hoja zote zinazotolewa na mkaguzi huyo zinafungwa kabla hata ya kuja mkaguzi wa nje.

Akizungumza hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka katika kikao cha baraza la Madiwani wilayani Ludewa kilicholenga kujadili majibu ya hoja na mpango kazi wa utekelezaji wa hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo katika halmashauri hiyo ilikuwa na hoja 19 huku hoja 7 kati ya hizo zikiwa zimefungwa kwa kipindi cha mwezi

Mei mwaka huu na kupelekea kusalia hoja 12.

Ameongeza kuwa kufanya kazi kwa ushiririkiano na mkaguzi wa ndani pia husaidia kuweka sawa taratibu mabalimbali ambazo zimekuwa zikikiukwa  na kumrahisishia kazi CAG pindi anapokuja kufanya ukaguzi wake huku akiwasisitiza kufanya vikao vya kisheria na kujadili hoja zote ambazo zimekuwa zikiibuliwa.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sunday Deogratias amesema amepokea ushauri na maagizo hayo yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuleta matokeo mazuri kwa miaka ijayo.

" Yote yaliyozungumzwa nimeyapokea na

tunaahidi kwenda kuyafanyia kazi ili kuweza kupunguza idadi ya hoja kwa miaka ijayo ama ikiwezekana kutokuwepo hoja kabisa". Amesema Deogratius.

Amesema katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2021/2022 halmashauri hiyo ilikuwa na hoja 19 ambapo hoja 10 zimefanyiwa kazi na kufungwa na kubakisha hoja 9 huku hoja za miaka ya nyuma zikiwa ni hoja 6 ambazo hoja 3 zilifungwa na kubakiwa na hoja 3.

 Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Wise Mgina amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo halmashauri hiyo imekuwa ikipata hati safi hivyo watahakikisha wanaendelea kupata hati hiyo safi kwa miaka mingine ijayo.

Hata hivyo katika  kupitia hoja hizo kwenye kikao hicho idara ya ardhi imeonekana kuwa na hoja nyingi na hasa katika suala la urasimishaji, ikifuatiwa na idara ya mweka hazina, mazingira, idara ya afya, ujenzi pamoja na idara ya manunuzi.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.