Leo asubuhi, tarehe 2 Desemba 2024, Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Eng. Elizabeth Sway, imefanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Wahandisi hao walipata fursa ya kusaini kitabu cha wageni na kupokelewa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka.
Katika mazungumzo yao, Eng. Sway alimueleza Mhe. Mtaka kuwa ziara yao mkoani Njombe inalenga kutembelea shule za sekondari na kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi. Juhudi hizo zinafanyika kupitia Mradi wa Student Support Program (SSP), unaolenga kuwajengea wanafunzi uelewa na shauku ya kuchagua taaluma za kihandisi na fani nyingine za kisayansi.
Mhe. Mtaka aliipongeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa jitihada hizo muhimu za kuinua elimu ya sayansi mkoani Njombe. Alisisitiza ushirikiano wa karibu kati ya serikali ya mkoa na ERB katika kuhakikisha wanafunzi wanapata motisha ya kusoma masomo ya sayansi kwa maendeleo ya taifa.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.