• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

WIZARA YA ELIMU YAVUNJA MKATABA NA MKANDARASI HERKIN BUILDERS LTD.

Posted on: October 6th, 2018

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imevunja mkataba na mkandarasi Herkin Builders anayejenga Chuo cha ufundi stadi cha Mkoa wa Njombe kilichopo eneo la Shaurimoyo wilaya ya Ludewa kutokana na kushindwa kukamilisha mradi kwa wakati hali iliyopelekea kuchelewesha utoaji huduma na kuitia Serikali hasara.

 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ametangaza kuvunjwa kwa mkataba huo leo alipofanya ziara katika eneo la mradi na kukuta hakuna kazi inayoendelea zaidi ya kuchimba msingi.

"Mkandarasi huyu amekabidhiwa kazi Novemba 15, 2016 na alitakiwa akabidhi kazi hiyo Septemba 10, 2017 hajakabidhi Serikali ikamuongezea muda mara mbili lakini hata muda ulioongezwa hakuna atakachofanya, hali halisi inaonekana tunavunja mkataba huu leo,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

Ole Nasha amesema hatambui tathmini ya Mradi iliyofanywa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na kumtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo ndani ya wiki moja kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathmini ya mradi huo.

"Ninyi VETA ndio mmeendelea kusisitiza kupewa kandarasi kwa kampuni hii pamoja na kuonyesha udhaifu katika kazi kadhaa ambazo amewahi kufanya na kuharibu bado ninyi mnafanya tathmini ya mradi hadi ilipofikia jambo hili halikubaliki na kampuni hii haifai kupewa kazi” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

Awali Mhandisi wa mradi kutoka VETA makao makuu Peter Sizya alimweleza Naibu Waziri tathmini iliyofanyika inaonesha kazi imetekelezwa kwa asilimia 6 ambapo zaidi ya milioni 590 zimetumika kumlipa mkandarasi.

Gharama za ujenzi wa mradi wa chuo hicho ni zaidi ya shilingi bilioni 9 na unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa kutumia fedha za mkopo kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na fedha za ndani.

Christopher philemon

Afisa habari Mkoa

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • DR. MICHAEL HAULE WA NM-AIST AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

    June 25, 2025
  • MWEKEZAJI NEIL GOODTILLERE WA BROWNS PLANTATION AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

    June 25, 2025
  • MAFUNZO MAALUMU KWA MADEREVA WA TAASISI ZA SERIKALI YAENDELEA MKOANI NJOMBE.

    June 14, 2025
  • MKUU WA MKOA WA NJOMBE MHE. ANTHONY MTAKA ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA MZEE MONGELLA JIJINI DAR ES SALAAM.

    June 04, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.