WAZIRI wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema Sekta ya Kilimo nchini itaweza kukua zaidi endapo Vijana nchini watatumiwa kama Nguvu Kazi katika kujishughulisha na mazao matano ya kimkakati ili kuchochea kasi ya uzalishaji hapa nchini.
Alisema hayo juzi mjini hapa alipotembelea mashamba ya Wakulima wa Majani ya Chai katika Kijiji cha Lwangu, Kata ya Uwemba mkoani Njombe,kikiwemo kiwanda cha Uniliver kilichopo hatua ya mwisho ya kukamilika kitakachosindika Chai ili kuwainua kiuchumi wakulima.
Alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa Vijana zaidi ya milioni 12 hapa nchini, lakini Vijana asilimia 56 tu ndiyo wanatengeneza Nguvu Kazi katika uzalishaji na bado hawana ajira.
Waziri Jenister alipongeza jinsi ambavyo shughuli za kilimo cha chai zinavyoendelea katika mashamba hayo kikiwemo kiwanda hicho, kwani kimeweza kusaidia kuongeza kupatikana kwa ajira kwa vijana mbalimbali mkoa wa Njome.
“Vijana ni kama milioni 12 na kitu, kwa hiyo vijana wanatengeneza asilimia 56 ya Nguvu Kazi yote tuliyonayo kwenye nchi yetu, lakini na vijana wengi pia hawana ajira na tunasema kwamba ajira siyo lazima iwe ajira rasmi, wanaweza kuajiriwa pia kwenye sekta ya kilimo,” alisema Jenister.
Aidha Waziri Jenister alisifu jitihada za vijana wanaofanya shughuli za uendeshaji wa Bodaboda na kisha kutenga muda wao mwingine kwenda kujikita kwenye uzalishaji wa majani ya chai, baada ya kuelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri namna ambavyo mwitikio ulivyokuwa mkubwa wa Vijana wanaojishughulisha na uendeshaji wa Bodaboda kutumia muda mwingine kufanya shughuli za kilimo hicho.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT), Geofrey Kilenga alisema Kilimo cha Chai nchini kinaweza kupanda kutoka tani elfu 35 ambazo zimekuwa zikizalishwa kwa miaka zaidi ya kumi ikilinganishwa na nchi ya Kenya ambayo imekuwa ikizalisha tano laki nne na nusu iwapo wataalam wa kilimo wataendelezwa.
“Chai ni zao la kimkakati, Tanzania tunazalisha wastani wa tani Elfu 35, lakini wataalam wakifundishwa wanaweza kufanya kazi kwa kushirikiana kati ya ubia wa Sekta binafsi na Serikali,” alisema Kilenga.
Akizungumzia suala la kuhakikisha kilimo cha chai kinaweza kumnufaisha zaidi mkulima kiuchumi, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri alisema wakulima wa chai wamekuwa na mwamko mkubwa hivi sasa mkoani Njombe ikiwemo kujiunga katika ushirika wa pamoja, lakini changamoto kubwa inayowakuta kwa sasa ni kukauka kwa baadhi ya mashamba hasa kipindi cha miezi ya Septemba, Oktoba na Novemba na kuiomba Serikali kuangalia jinsi ya kusaidia kuwepo kwa umwagiliaji wa mashamba ya chai kipindi cha kiangazi.
“Asilimia 66 ya Chai tuliyoipanda inaweza kukauka kipindi cha kiangazi, tunaiomba serikali itusaidie katika kuanzisha kilimo cha umwagiliaji,” alisema Ruth.
Meneja wa Kampuni ya NOSC,inayojishughulisha na ununuaji wa majani ya Chai kwa wakulima wadogo, Filbert Kavia alimweleza Waziri Jenister kuwa kutokana na jinsi Vijana na Wanawake kuwa na mwitikio wa kujiunga katika mashamba ya ushirika
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.