Wahandisi wanaosimamia miradi ya ujenzi nchini wametakiwa kufanyakazi kwa kuzingatia weledi ili kuepusha taifa kupoteza fedha nyingi katika miradi hiyo ya maendeleo ambayo imekuwa ikihujumiwa kutokana na kukosa uaminifu.
Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2018 CHARLES KABEHO wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe mara baada ya kukagua na kuzindua miradi ya maji na barabara itakayosaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na ufasirishaji wa mazao kutoka shambani.
Mwenge wa uhuru ukiwa katika halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe mara baada ya kumaliza mbio zake katika halmashauri ya mji wa Makambako umezindua miradi ya maji, barabara, daraja pamoja na kituo cha afya.
Akizindua mradi wa maji katika kijiji cha Isindagosi Kabeho aliwataka wahandisi na wakandarasi kuwa waadilifu katika kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kuzuia taifa kupata hasara.
"Taifa Limekuwa likipata hasara kubwa katika miradi yake hali iliyokuwa Inapelekea fedha nyingi kupotea... Niwatake wahandisi kufanya kazi kwa uzalendo ili tusiendelee kupoteza fedha zetu" alisema Kabeho.
Wakazi wa kijiji hicho wamesema mradi huo utatatua shida ya upatikanaji wa maji safi na salama hali iliyodumu kwa kipindi kirefu
Aidha,Kabeho alizindua na kukagua ujenzi wa barabara ya Imalinyi Kidugala hadi Masilu kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilomita 26, ambapo wakazi wa kijiji cha Imalinyi walisema kukarabatiwa kwa barabara hiyo itawasaidia kusafirisha mazao.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa 2018 alikagua na kuzindua mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana, madarasa matatu na matundu sita ya choo katika shule ya sekondari Wanike.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.