Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO)Bw. Jose Graziano da Silva amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Shirika hilo lipo tayarikushirikiana na Tanzania kufanya mageuzi katika kilimo kwa kuwezesha uzalishajiwa mazao na viwanda vya mazao hayo.
Bw. Jose Graziano da Silva amesema hayo tarehe 06 Septemba, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada yakufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli na kumshukuru kwa ushirikiano mzuriambao shirika hilo limeupata kwa kipindi cha miaka 40 ya uwepo wake hapanchini.
Akitoa mfano wa nchi yake ya Brazil Bw. JoseGraziano da Silva amesema Tanzania inaweza kupata manufaa makubwa ya kuongezauzalishaji wa chakula, kuuza nje ya nchi, kuzalisha ajira na kukuza pato laTaifa kupitia mapinduzi yatakayotokana na kuunganisha kilimo na viwandavikiwemo vya kusindika nyama na samaki kwa kuwa fursa zipo nyingi.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuruBw. Jose Graziano da Silva kwa kuja nchini na amemhakikishia kuwa Serikaliitaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake FAO, huku akitilia mkazodhamira yake ya kutaka ushirikiano huo uelekezwe katika ujenzi wa viwanda vyakuzalisha bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.
“Tanzania ina maziwa mengi, ina ukanda wabahari wenye urefu wa kilometa 1,422 na ina mito mingi ambayo inaweza kuwekezwaviwanda vya samaki, inashika nafasi ya pili kwa mifugo Barani Afrika, hivyotunahitaji kujenga viwanda vya nyama.
“Asilimia 75 ya nguvu kazi ya Taifa nivijana ambao wanauwezo wa kuzalisha mazao mengi ya kilimo tunahitaji viwanda,uchumi wetu ni mzuri na unakua kwa wastani wa asilimi 7.1 na mengine mengi, kwahaya yote tunahitaji wadau ikiwemo FAO tushirikiane kutumia fursa hizi”amesema Mhe. Rais Magufuli na kuahidi kuwa Serikali yake imejipanga kusimamiamiradi yoyote itakayoletwa nchini ili itekelezwe kwa uadilifu na ubora wa haliya juu.
Wakati huo huo, Mhe. RaisMagufuli amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MwalimuNyerere Mzee Joseph Butiku Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya mazungumzo hayo Mzee Butiku amempongezaMhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuongoza Serikali ambapo katikakipindi kifupi amesimamia vizuri nidhamu, watu kufanya kazi, kupiga vitarushwa, ulipaji wa kodi na amemtaka asirudi nyuma kwa kuwa nchi inakwendavizuri.
“Mimi nimefanya kazi hapa Ikulu kwa miaka23, Mwl. Nyerere alijenga misingi mizuri, lakini huyu Rais Magufuli ameisimamiavizuri sana, unapofanya mambo kama haya, lazima hapa nyumbani na huko njekutakuwa na maneno, mazuri sikiliza, ya hovyo achana nayo” amesisitizaMzee Butiku.
Katika hatua nyingine, Mhe. RaisMagufuli ameagana na Balozi wa China hapa nchini anayemaliza muda wake Mhe.Dkt. Lu Youqing na kumshukuru kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya katikakipindi cha miaka mitano aliyokuwepo hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli amesema katika kipindi chakeMhe. Dkt. Lu Youqing ametoa mchango mkubwa katika kuendeleza na kukuza zaidiuhusiano na ushirikiano kati China na Tanzania, uliofanikisha kuongezauwekezaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu,elimu, kilimo, afya na kukuza biashara ambapo wafanyabiashara wengi wa China wamekujakuwekeza nchini, mambo ambayo yamezalisha ajira na kukuza pato la nchi.
Mhe. Dkt. Magufuli amemuomba Mhe. Dkt. Lu Youqingkuendelea kuitangaza vyema Tanzania nchini China, ambako anakwendakushughulikia masuala ya uchumi na kwamba anaamini atatumia nafasi hiyokuhimiza wawekezaji na wafanyabiashara wengi zaidi wa China kuja kuwekeza hapanchini.
“Mhe. Balozi Dkt. Lu Youqing Watanzaniahatutakusahau kwa mchango wako, wewe ni ndugu na rafiki yetu, tunakushukurusana kwa yote uliyoifanyia nchi yetu, naomba nikuhakikishie kuwa kazi nzuriuliyoifanya tutaiendeleza na tutashirikiana na Balozi mpya atakayekujakuendeleza pale ulipoachia” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Dkt. Lu Youqing amemshukuruMhe. Rais Magufuli kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi chote alichokuwepohapa nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwa Balozi mzuri wa kuinadi Tanzaniahuko nchini China.
“Mhe. Rais Magufuli nakushukuru sana, hapaTanzania ni nyumbani kwangu na nipo tayari wakati wote kutoa ushirikiano palenitakapohitajika kufanya hivyo kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini China amakutoka Serikalini hapa Tanzania” Amesema Dkt. Lu Youqing.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Septemba, 2017
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.